MAMBO HAYA
YATAKUSAIDIA KATIKA KUANZISHA BIASHARA YAKO.
Habari yako
ndugu msomaji wangu wa Nderingotz.blogsport.com,kama ilivyoada mwaka mpya ndo umeshaingia na kabla ya treni
ya 2015 haijaanza kushika kasi sana ,napenda kuwaletea mada moto moto juu ya kuinua
uwezo wako binafsi wa kuanzisha au kutunza biashara yako..
Watu wengi wamekua wakikalili mtazamo hasi
juu ya ni biashara gani inalipa zaidi?leo napenda kukupa jibu kuwa,biashara
inayolipa ni ile ambayo una wazo nayo thabiti na pia inahitajika na mazingira
yako husika,la msingi ni zile skills ambazo zitakuwezesha kuwa mpana(bolds),si
ajabu hata wewe ukiwa unazarau aina Fulani ya biashara kutokana unaangalia
maisha husika ya wafanya biashara hizo.Napata kujiuliza biashara ya
mandazi,nazi,maji,nyanya inakuaje zinaweza kuzalaurika wakati zinamwingizia
pato kubwa mzee Said backhressa,naomba liwe swali na kwako pia.
Bila kuchoka hatua kwa hatua twende pamoja
ktk kudiscus mawazo yafuatayo juu ya kuanzisha na kuipanua iashara yako.
WAZO
LA BIASHARA;hii ndio mzizi mkuu wa biashara,kama hutokuwa na wazo thabiti
ambalo litaibeba biashara yako katika kipini Fulani cha miezi,miaka au
milele,basi utakua umefeli ktk yote,hivyo hii ni sehemu makini na inayotaka
utulivu mkubwa,mwombe MUNGU akusaidie upate wazo bora,ikiwezekana tafuta
ushauri kwa watu wenye ufahamu juu ya mambo ya biashara kwa mf;mr.Jonathan
Kisingi wapate cha kukushauri juu ya wazo lako.
UTAFITI WA KINA;hii ni hatua nyingine MUHIMU katika
kuanzisha biashara yako,yaweza kabisa wazo lako baada ya kufikia hatua hii ya
mwanzo likapata upinzani,game likaonekana ni gumu.Usikate tama jaribu wazo lingine
ambalo litakuwa linakurizisha wewe kuanza hiyo biashara.Fanya utafiti wa
kutosha kwa wateja na kwa mzalishaji anaetoa hizo bidhaa.
HALI YA UCHUMI YA WATEJA WAKO;yaweza kuwa umefanikiwa ktk kipengele
cha kwanza na cha pili lakini ukakosa kukumbuka kitu hiki muhimu``HALI YA
WATEJA’’je, bidhaa yako iko mahali sahihi kulingana na aina ya bidhaa kulingana
hadhi ya wateja husika,kwa mf;biashara ya magodoro japo inaweza kulipa sana
sehemu ambazo watu wanaendelea kuhamia lakini ukienda kuipeleka maeneo ya
polini sana,utakutana na watu wenye uwezo duni na wamezoea kulalia ngozi,haaaa ahaa itabidi uyagawe?hapo
kazi ipo………
ISOME
BIDHAA YAKO;hii ndio udhaifu mkubwa kwa watoa huduma wengi hivyo kushindwa
kukidhi customer care principles.Mteja anajisikia furaha anapohudumiwa na mjuzi
wa bidhaa vizuri,hii itakuongezea umakini na kuonekana ni wa tofauti.
ENEO HUSIKA;hapa
tunawaangalia wale wajasilia mali wadogo kabisa ambao ndio wanaanza na mitaji
yao midogo.Suala la kodi ya pango inaweza kuruhusu uhai kwa biashara
yako?nadhani jibu lako ndio litakuongoza zaidi uendelea au kutafuta kwingine.
SHERIA ZA NCHI;hii ni jambo muhimu kuzingatia je, biashara hii ni sahihi kulingana na
sheria za nchi?si mnajua kuna baadhi ya bidhaa zile za kule R-chuga ahaa ni
noma sana wadau wa usalama wakurudisha nyuma.Tafuta vibali juu ya biashara
yako,japo nanyi serikali legezeni kidogo gharama ya hivyo vibali.
MTAMBUE
MTEJA WAKO;hii ni silaha hadimu sana kwa mfanyabiashara,wateja
wamegawanyika kwa tabua zao kuzijua itakua ni msaada kwako ktk
kuwahudumia.baadhi ya hizo tabia ni;-
Ø AGGRESSIVE,huyu huwa ni mtu wa
makelele mara zote awapo na tatizo juu ya bidhaa yako,huja kwa kufoka ili
wengine wasikie nini asemacho,chukua hatua ya kukaa kimya mara amalizapo mjibu
kwa upole na umwombe msamaha,kumb;neno msamaha kwa mwenye hekima
litamwinua bali kwa mpumbavu litamwangamiza.
Ø RIP-OFF,huyu ni aina ya wateja ambao
huwa hupenda kupata vitu ambavyo kimsingi si haki wao kupatiwa,hii inatokea
mara inapotokea dosari ktk utoaji wako wa huduma.
Ø HIGH ROLLER,Hawa ni aina ya wateja
ambao huangalia ubora wa bidhaa bila kujali ni gharama kiasi gani watatumia
kuweza kuipata,hawa ndio wateja ambao sio wasumbufu lakini changamoto kubwa
huja pale utakapobadili zile qualities za bidhaa zako,wakihama hawarudi.
Ø MEEK,hawa ndio wabaya kabisa,huwa
kama kondoo pale wanapopata huduma mbaya,hawatokwambia dosari zako bali
wanaenda kuchafua huko waendako.HAWA NDIO WABAYA ZAIDI.mara zote ni vigumu
kujulikana.
MAONO;hili ni jambo linalolipulizia pumzi
ya uhai kila kukicha biashara yako,kuwa na maono makubwa juu ya biashara yako
ukiambatana na kuita majina makubwa makubwa hiyo biashara yako kama,KISINGI
ENTERPRISSES LTD,KISINGI RESTAURANT,KISINGI INDUSTRY na mengine mengi kama
hayo,hii itakusaidia kuipatia nyama wazo lako.
IMANI;imani ni jambo la msingi ktk biashara
yoyote,kuwa na muda wa kuombea biashara dhidi ya kila hila ya adui,na pia kuwa
na utaratibu wa kupenda kutoa sehemu ya mapato yako kama sadaka.
TAMBUA CUSTOMER CARE TIPS;Mtambue mteja ni nani?na ni njia gani
bora za kumhudumia mteja jinsi ipasavyo….hapa pia unaweza kutafuta wataalamu
kwa maana ni somo pana.
FANYA MATANGAZO;hili ni jambo la wazi,biashara yoyote
inahitaji matangazo ya kutosha ili ipate kuweza kupiga hatua za haraka.agalizo;usitumiwe
gharama nyingi mno ktk matangazo.
NA PIA KUNA
MAMBO MENGINE YA MSINGI KAMA;
NIZAMU KATIKA MATUMIZI YA PESA NA
KUWEKA AKIBA,
UVUMILIVU KATIKA BIASHARA;Hii ni kweli kabisa wahenga husema
mvumilivu hula mbivu,usiwe na kupenda mafanikio ya haraka pata muda wa kutosha
wa kukaa kwenye game hii itakusaidia wewe kupata fulsa zaidi kutokana na hiyo
biashara.
BE BOLDS(Tafuta fulsa nyingie);mara nyingi mjasiliamali hodari ni
Yule anayeweza kujipanua kwenye makundi mengine mbali mbali,hii itakupatia
uhakika endapo hata biashara moja ikidolola nyingine itaendelea kufanya vizuri.
WEKA AU TUNZA NYARAKA ZA BIASHARA
YAKO;
PATA MUDA WA KUTOSHA WA KUITUMIKIA
BIASHARA YAKO;ni
ukweli kabisa mzazi asiyekua na muda wa kutosha wa kuwalea watoto wake,si jambo
la ajabu hao watoto kupoteza dira.Ni vyema ukapata muda wa kutosha wa kuitunza
biashara yako,kwa maana ni wewe uliye na malengo na maono juu ya hiyo biashara.
Usichoke
kutembelea blog hii,nderingotz.blogsport.com{HOME OF UPDATED AND
INSPIRATION NEWZ}
PIA USIACHE
KUTOA MAONI YAKO HAPA CHINI;
kwa mawasiliano ;+255 654 342 752
SINCE YOU KNOW THESE,NOW GO OUT THERE AND TREAT
YOUR CUSTOMER RIGHT.