Kijana achinja familia na kuwala
Kijana achinja familia na kuwala
KIJANA
mmoja raia wa Hong Kong amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mauaji,
kutawanya viungo vya nduguze, kuwanyunyizia chumvi na kuwapika.
Mtuhumiwa huyo ana umri wa miaka 31 na ametambulika kwa jina la Henry Chau.
Kijana
huyo aliibua hisia za walio wengi katika kesi ya namna yake mnamo 2013
wakati kichwa cha mama yake mkubwa pamoja na baba yake vilipobainika
kuhifadhiwa katika majokofu mawili tofauti.
Kesi hiyo iliendeshwa
katika mahakama kuu ya nchini humo iliyopo mjini Hong Kong ambapo
alielezea jinsi alivyokuwa akiwaua nduguze.
Chau hutekeleza
mauaji hayo ambapo kwanza huua, pili hutawanya viungo vya maiti na kisha
huwanyunyizia chumvi ili kuongeza ladha ya nyama katika miili hiyo.
Kwa
mujibu wa Shirika la habari la Xinua, Chau alisema kuwa anafanya hayo
yote kutokana na matokeo ya mapenzi yake kwa nyama choma ya kitimoto.
Chau
alisema kuwa nyama hiyo ya binadamu ikishaiva ama kuchomwa huwa
anafunga nyama hiyo katika makasha ya chakula pamoja na ubwabwa.
Polisi walipofanya upekuzi katika nyumba yake walikuta baadhi ya viungo vya binadamu katika chombo cha kuhifadhia taka.
Akitoa
hukumu dhidi ya kesi hiyo, jaji Michael Stuart-Moore alimuelezea Chau
kama mbinafsi mwenye msongo wa mawazo kutokana na mafanikio mabaya ya
maisha yake na asiye na huruma kwa wengine.
Chau, alihukumiwa
adhabu mbili ikiwa ni pamoja na kifungo cha maisha jela na miaka tisa na
miezi minne kwa makosa mawili tofauti kwa kuvunja sheria ya kuzika
miili ya familia yake isivyo kawaida kosa ambalo alilikiri baadaye.
Hapo awali rafiki wa Chau alikuwa akihusishwa katika mauaji hayo ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita alikutwa hana hatia.
Taarifa
za kupotea kwa wanafamilia wa Chau zilipoibuliwa, Chau alidanganya kuwa
jamaa zake walikuwa wamesafiri lakini baadaye alijisahau na kumuandikia
rafiki yake kupitia ujumbe mfupi wa simu kwamba aliwaua jamaa zake.
Chau
mwenyewe hujiita mwendawazimu katika ujumbe aliokuwa akiwatumia watu
wake wa karibu alisema katika ujumbe huo kuwa hawezi kumuonea huruma mtu
yeyote kutokana na maumivu aliyopitia wakati wa makuzi yake utotoni
mpaka anakuwa mtu mzima.
Chau anasema kuwa aliamua kuwadanganya polisi ili apate wasaa wa kuwaaga marafiki zake
No comments:
Post a Comment