Tuesday, December 23, 2014
JINSI YA KUJIKOMBOA KIMAISHA KWA VIJANA
Jinsi ya Kujikomboa Kimaisha Kwa Vijana
Hapa chini kuna muongozo wa kumfanya kijana afanikiwe kimaisha.
UNACHOAMINI
Njia ya kwanza ya kijana kujikomboa inaanzia kwenye kile anachoamini
katika maisha yake. Katika hali ya kawaida mwanzo wa imani ya mwanadamu
hutoka kwa wazazi wake na wakati mwingine mazingira atakayokulia.
Kwa mfano, wengi tumekuwa na dini kwa sababu tulizaliwa na wenye dini,
kwa maana hiyo hata tunachokiamini hatukuchagua kwa akili zetu wenyewe.
Kwa msingi huo, kama kuna walio na dini mbaya (nataja tu), wengi wao
wameponzwa na kile walichorithishwa na wazazi wao.
Hali iko hivyo kwenye njia hii ya kwanza ya kijana kuelekea kwenye
mafanikio. Wengi tumezaliwa na kurithishwa imani ya kutofanikiwa. Wazazi
wetu walitulea kwa kutuambia maisha ni magumu, hatuwezi kufanikiwa,
sisi ni masikini, duni na maneno kama hayo ya kukatisha tamaa.
Hata hivyo, walifika mbali zaidi ya hapo kwa kutuita majina “mbwa,
nyani, wajinga, wapumbavu, vichaa na waliolaaniwa. Ushahidi wa hili upo
mpaka leo, kuna wazazi wanawaita watoto wao majina ya aina hiyo.
Kwa hiyo, tukakua tukiamini kuwa sisi ni watu duni ambao hatuwezi
kufanikiwa na kama tukiona mafanikio sehemu yoyote tunakuwa na mawazo
kuwa, hiyo ni zawadi ya akina fulani wa ukoo mwingine, lakini siyo sisi.
Mawazo ya vijana wengi leo yanaamini kuwa, umasikini ni mzigo mkubwa
usiokuwa na ufumbuzi. Kitaalamu mtu anapokuwa na mawazo ya
kutokufanikiwa hawezi kufanikiwa kwa sababu mafanikio huhitaji nguvu na
nguvu za mwili haziwezi kujitokeza kama hazikuvutwa kufanya kazi.
Kwa msingi huo, ili mtu aweze kufanikiwa lazima mawazo yake yakubali
kuwa mafanikio ni sehemu ya lazima katika maisha. Jambo hili haliwezi
kutokea mpaka kijana mwenyewe aliyelelewa kwenye mawazo ya kushindwa
apigane vita na mawazo ya kutofanikiwa na kuyashinda.
Njia pekee ya kujikomboa na mawazo mgando ni kufuta na kupuuza kauli
zote alizoambiwa na wazazi wake kuhusu maisha magumu na kuanza kuamini
kuwa, maendeleo ni yake na kwamba muda unahitajika kuyafikia.
Nakushauri kijana mwenzangu kuanzia leo uyakatae mawazo ya kushindwa na
kukubali udhaifu wako kwamba huwezi kufanikiwa kwa sababu yoyote ile,
sema LAZIMA UFANIKIWE KWA KUWA UWEZO HUO UNAO.
UNACHOTENDA
Ukiangalia tabia ya maisha ya mwanadamu utagundua kuwa anafahamu mambo
mengi sana, lakini hatendi sawa na ufahamu wake. Naamini hata vijana
wanajua njia za kufanikiwa, lakini hawazifuati.
Binafsi kuwafundisha watu kile wanachokifahamu ni sawa na ujinga. Kamwe
siwezi kutumia muda wangu kuwaambia vijana ili waendelee wanahitaji
kufanya biashara, kuajiriwa, kujiajiri kulima, kwani kufanya hivyo ni
kukosa shabaha ya elimu.
Ukitaka kuthibitisha hili zungumza na vijana wanaoishi maisha magumu
uone kama hawatakuorodheshea njia zaidi ya 100 za kufanikiwa kimaisha!
Kumbe tatizo lao si kujua bali ni kutenda ambako ndiyo njia ya kuelekea
kwenye mafanikio.
Wewe kama kijana jaribu kukumbuka ni biashara, mradi, kazi gani
uliyokwishaiwaza na mpaka leo hujaanza kuifanya kwa sababu ambazo
hazifahamiki? Miongoni mwa watu wenye tatizo hili wapo ambao si tu
kwamba wana wazo, wana fedha, nguvu bali wana uwezo wa kufanya mambo
yakawezekana, lakini wamejikuta hawafanyi yale wanayoyaweza na hivyo
kubaki watumwa wa umasikini wakiamini tu kuwa, ipo siku wataanza na
kufanikiwa.
Tatizo kubwa katika mgando huu wa mawazo ni woga wa kushindwa na ugumu
wa kuanzisha jambo. Wanasema waswahili ‘MWANZO MGUMU’ hata hivyo haiwi
sababu ya wengi kushindwa kufanya mambo kwa kuhofia kukutana na ugumu.
Watu wengi waliofanikiwa duniani ni wale ambao walikuwa tayari kuingia
katika hatua hii muhimu ya kutenda yale waliyoyawaza na kuyathibitisha
kuwa yatasukuma mbele maisha yao.
Wote tunajua mwanzo wa kila kitu ni wazo, lakini mawazo yasiyokuwa na
matendo ni upuuzi! Vitu ambavyo vimekuwepo duniani na vitakavyokuwepo
baadaye vitatokana na ushirikiano wa hatua hizi mbili yaani KUAMINI NA
KUTENDA. Ni wakati wako wa kuamini au kugeuza mawazo yako kuwa vitu
halisi.
Umewaza sana kujenga nyumba mbona hujaanza kujenga? Unasubiri nini
kuanza biashara uliyoifanyia utafiti na ukagundua kuwa itakuingizia
kipato. Nani kakuzuia usipange chumba chako na kuanza maisha yako? Amka
na uanze kufanya yote uliyoyawaza!
UNACHOCHAGUA
Katika hali ya kawaida mwanadamu wa kawaida ana mahitaji mengi
yanayotoka kwenye vitu vingi pia. Ukihitaji mchumba kwa mfano,
itakulazimu hitaji lako likutane na wingi wa wachumba tofauti tofauti.
Changamoto utakayokutana nayo wakati utakapokuwa unataka kutenda
ulichoamini ni kuchagua.
Tambua kuwa chochote utakachotaka duniani hakiko peke yake, ukienda
sokoni kununua nyanya, utakutana na mafungu mengi ya bidhaa hiyo kiasi
cha kukufanya utumie akili kuchagua fungu moja au mawili unayohitaji.
Kuwepo na vitu vingi vya kuchagua kama nilivyosema ni moja kati ya
tatizo kubwa linalowafanya vijana wengi washindwe kufanikiwa kimaisha
kutokana na kutokuwa makini wakati wa kuchagua. Wapo ambao wameshindwa
kuendelea kwa sababu tu walichagua wake wabaya, biashara, fani, kazi,
kilimo kibaya na mambo mengine.
Inawezekana kabisa pengine hata mambo ambayo yanakuendea kombo leo
yametokana na kosa lako la kuchagua. Ushauri wangu ni kwamba kila mtu
anayetaka kufanikiwa kimaisha lazima ahakikishe mambo anayoyachagua yawe
ni yale aliyoyahakiki kuwa yanafaa.
TUNACHOPATA
Katika hali ya kawaida hakuna mtu anayetafuta kila siku asipate, hili
halina ubishi, labda kinachoweza kuwa tofauti ni kiwango cha kupata.
Saturday, December 6, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)