Mafanikio
ni mchakato, ili uweze kuona ndoto zako zinatimia, kuna mchakato
inabidi uupitie. Kutimiza ndoto zako kwanza kuna mambo mawili unatakiwa
uyaangalie ndani yako mambo hayo ni a) Dhamira b) Beliefs
-
DHAMIRA(DESIRE)
Kweli umedhamiria? Ukijichunguza
toka kilindi cha moyo wako, umeamua kweli unataka kutimiza ndoto yako,
kiwango ni mpaka ndani yako kuwe na moto wa kutosha, utakao kupa nguvu
ya kukusukuma kuelekea kwenye kutimiza ndoto yako, kama hujafikia
kiwango hicho, hakikisha unaikuza hiyo dhamira, ufike kwenye kiwango cha
kusema haijarishi nini nitakutana nacho chiani, nimeamua kutoka ndani
kwamba nahitaji kuona ndoto yangu ikitimia.
-
HALI YAKO YA NDANI(BELIEFS)
Neno belifs hapa haina maana ya
belifs ile inayojulikana na wengi ya imani ya dini, NO. Belifs hapa
ninamaanisha ni taarifa zilizowekezwa ndani yako, kwa njia mbali mbali
na wazazi wako hasa ukiwa na umri kati ya 0-12 years, watu au jamii
inayo kuzunguka, mfumo wa elimu uliyopata, vyombo vya habari n.k. Mambo
hayo yote yametengeneza mtazamo Fulani wa maisha ndani yako, na jinsi
uanvyo yaona na kuyatafsiri maisha, na taarifa hizi ndizo zinatangeneza
mfumo wako wa kufanya maamuzi na mara nyingi maamuzi au hatua utakazo
chukua zinategemea taarifa hizi zilizo ndani yako, taarifa hizi ndizo
zinatengeneza picha uliyokuwa nayo kuhusu maisha, na ndiyo inapelekea
aina ya maisha uliyokuwa nayo, hiyo ndiyo tunaita BELIEFS. Maisha yako
uliyonayo sasa hivi ni matokeo ya jinsi ulivyo ndani, nini kimewekezwa
ndani yako, aina gani ya beliefs uliyonayo, belifs yako.
Sasa unapotaka kutimiza ndoto
uliyokuwa nayo, nilazima utathmini that kind of belief uliyonayo sasa
hivi inaweza kweli kui support ndoto yako? Hamna namna utaweza ku
achieve ndoto hiyo uliyonayo bila ya kubadilisha baadhi ya beliefs
ulizokuwa nazo, wengine wanaita reprogramming of your mind, watu wengi
wamekwama kwenye maisha, si kwasababu hawana ndoto, si kwasababu
hawafanyi kazi kwa bidii, lakini moja ya sababu kubwa ni beliefs
walizonazo, hizi zimekuwa ni hand break kwenye maisha yao, kutimiza
ndoto zao wanahitaji kubadilisha hizi beliefs.
No comments:
Post a Comment