Tuesday, November 25, 2014
SIRI YA UTAJIRI
Kwa nini watu wengine ni matajiri ?
Watu wengi wanajiuliza, "Siri ya utajiri ni nini?" Jee ni mbinu gani
zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni
kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa
namna ambayo daima panakuwa na ziada na faida. Kwa bahati mbaya sana,
elimu hii haifundishwi darasani ila wanayo wafanyabiashara wachache na
kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri na huendelea kuificha.
Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza kuigundua siri ya
utajiri. Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze kufanikiwa na wapate
manufaa kwa kununua kitabu hiki nimeamua kuiweka siri hii wazi:-
- Siri ya kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi unaojipa, yaani
unaoweza kuitoa ziada na faida.
- Siri ya pili ya kuelekea kwenye utajiri ni kujifunza na kujenga tabia
ya kuweka akiba
- Siri ya tatu ni kuwekeza fedha hizo za akiba katika vitega uchumi
ambavyo vinazalisha faida endelevu.
- Siri ya nne ni kujifunza namna ya kufanya biashara na kuanzisha
biashara yako ili iwe indelevu.
Kuna njia mbili za namna ya kupata utajiri zenye uhakika. Njia ya kwanza
ni njia ndefu ambapo wataalamu na watafiti wa masuala ya fedha
wameigundua njia hii ni rahisi kuifuata kwa sababu haihitaji uwe na
kipato kikubwa, wanashauri kwamba ujenge tabia ya kuweka akiba, anza
kuweka akiba ya T.shs 1,000 kila siku sawasawa na TShs 30,000 kwa mwezi,
matokeo yake ni kwamba kama utaweka akiba yako kwa kipindi cha miaka 65
bila riba yoyote utakuwa na akiba TSshs 23,725,000 (Milioni Ishirini na
Tatu Mia Saba Ishirini na Tano Elfu). Kama utawekeza fedha hiyo na
kupata riba ya asilimia 10% kwa kila mwaka itazaa na kukuletea TShs
2,750,000,000 (Bilioni Mbili na Milioni Mia Saba Hamsini). Hesabu hii
inaweza ikakutisha na usiamini macho yako lakini hiyo ni siri ya nguvu
ya hesabu na riba kama alivyozielezea mwanafizikia Enstein kwamba katika
dunia hii hakuna kitu chenye nguvu kama hesabu za riba. Pengine njia
hii inaweza kuwa ni ndefu sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wetu
hatuwezi kusubiri muda mrefu. Hivyo tungependa kuwa na mafanikio ya
kiuchumi kwa haraka. Lakini nasisitiza kama kipato chako ni kidogo anza
leo kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku.
Dundulizo la akiba hii hukutiririshia utajiri bila wewe kukusudia kwani
utaweza kukidhi hitajiko la ghafla kama kuugua safari ya dharura gharama
za likizo na hata kutumia mbinu hii kama mpango wa elimu kwa watoto
wako iwapo utawaanzishia hivi mara tu kila mmojawapo anapozaliwa au
unaweza kuutumia kama upanga wa siku zijazo kwa mirathi ukianza hivyo
leo kwa kupangilia namna hiyo kwa kila kusudio lako la baadaye.
Hebu tuangalie njia ya pili.
- Njia ya pili ya mkato ni kuongeza kiwango cha kuweka akiba kama wewe
ni mtu mwenye shughuli za kuzalisha ziada. Kipato chako kinaweza kuwa
kinaongezeka kila mara. Badala ya kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku
jiwekee malengo ya kuweka akiba ya TShs 10,000. Anza kwa kutenga
asilimia 10% ya mapato yako hadi utakapofikia lengo la TShs 10,000 au
zaidi kwa siku. Badala ya lengo lako kutimia kwa miaka sitini na tano
(65) litatimia haraka zaidi. Kwa mfano ukiweka akiba ya TShs 10,000 kwa
siku kwa muda wa miaka sita na miezi sita bila riba yoyote utapata TShs.
23,725,000. Ukiwekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa
miaka sita na miezi sita utapata TShs. 33,917,505.78. Kama fedha hiyo
utaendelea kuweka akiba kwa riba hiyohiyo hadi kufikia muda wa miaka
kumi utapata TShs. 63,112,201.43.
Kwa kuwa kitu cha muhimu hapa ni kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo
katika kitegauchumi chenye kutoa faida kubwa, utajiuliza jee uwekeze
kwenye kitega uchumi chenye kutoa faida kiasi gani? Wataalamu wa mambo
ya fedha wanashauri kuwa uwekeze fedha yako kwenye kitegauchumi chenye
kutoa faida ya angalau asilimia 10% Kwa mfano unaweza kuwekeza kwenye
Akaunti ya TAJIRIKA ya Standard Chatered Bank" inatoa riba ya asilimia
kumi 10% pia unaweza kuwekeza kwa kununua hisa katika soko la hisa na
mitaji.
Kwa wastani wa watafiti wa masuala ya fedha viwango vya mapato
yatokanayo na hisa kwa gawio pamoja na kukua kwa mtaji ni zaidi ya
asilimia 11% ambayo ni makubwa kwa kiwango cha kawaida cha asilimia kumi
(10%).
Baada ya kueleza siri ya namna ya kupata utajiri nitazitaja njia zingine
ambazo zinaweza kukuwezesha kuwa tajiri.
1. Unaweza kurithi mali na fedha kutoka kwa wazazi wako. Hii ni njia ya
kubahatisha kwani watu matajiri siyo wengi na hivyo watoto wenye bahati
kama hii ni wachache pia.
2. Unaweza kusomea ujuzi au utaalamu katika fani yenye malipo mazuri na
kujiajiri mwenyewe. Kwa mfano, unaweza kusomea fani kama ya Uanasheria,
Uhasibu na Udaktari au ufundi / sanaa na kadhalika.
3. Unaweza kuanzisha biashara yako na kuiendesha ili kupata ziada kubwa.
4. Unaweza kuendeleza vipaji vyako na kuwa mwanamichezo au msanii wa
kulipwa.
5. Unaweza kutunga vitabu juu ya suala lolote unalolijua. Kwa mfano,
kama wewe ni mtu uliyebobea katika masuala ya muziki unaweza kutunga
kitabu kinachofundisha watu namna ya kuwa mwanamuziki. Watunzi wengi wa
vitabu ni matajiri wakubwa. Hii ni kazi unayoweza kuifanya mara moja
lakini ukavuna matunda yake kwa muda mrefu sana.
6. Unaweza kuwa mbunifu na kuanza kuuza mawazo yako au kutumia chombo
ulichokibuni kukuingizia fedha.
7. Unaweza kucheza bahati nasibu na kushinda. Tatizo hapa soko na wateja
wa aina hii ya huduma ni haba. Hiki ni kitu cha kubahatisha na
nimekitaja makusudi ili kuwapa onyo wasomaji kwani watu wengi wanapenda
sana kucheza michezo ya kubahatisha.
Uwezekano wa kutajirika kwa njia hii ni mdogo sana. Hivyo, nawashauri
wasomaji kuachana na njia hii ya kutafuta utajiri. Nawashauri wachague
njia yoyote inayofaa na inawezekana kwa kufuatana na mazingira
yanayomzunguka mtu husika. Mkulima au mfugaji anaweza kuzingatia fani
hii na kutajirika sana. Kwa kweli hakuna mipaka, hasa hapa kwetu
Tanzania kwa sababu ya wingi wa fursa za kuweza kujishughulisha na kuwa
tajiri.
Maelezo ya kina juu ya aina ya biashara au mbinu unaweza kuzitumia
kutafuta na kupata faida utayapata katika sehemu ya pili ya kitabu hiki.
Inawezekana kuwa tofauti kati ya mtu tajiri na mtu maskini inatokana na
kile tulichojifunza kutoka kwa wazazi wetu. Wazazi maskini huwaambia
watoto wao wajitahidi kusoma sana ili wapate maksi nzuri darasani na ili
baadaye waweze kupata kazi nzuri. Wakati wazazi matajiri huwapa watoto
wao elimu ya namna ya kutafuta fedha. Kwa kawaida tukiwa shuleni
tunapewa ripoti ya masomo. Katika maisha tunatakiwa kuwa na ripoti yetu
ya maisha nayo ni orodha ya mali tulizonazo ikiwa ni pamoja na elimu ya
kuzaliwa na ya kusomea na fedha taslimu zile zilizo katika hifadhi
mbalimbali.
Kwa kufuata tafsiri ya Umoja wa mataifa mtu masikini ni yule ambaye
kipato chake hakizidi TShs 1,000 kwa siku.
Inawezekana kuwa mfumo wa kifedha wa mtu maskini ni mfumo ambao humfanya
kutumia kipato chake chote kulipia matumizi huwa hana ziada wala uwezo
wa kuweka akiba hana madeni na hana mali.
Mfumo wa fedha wa mtu mwenye kipato cha kati ni mfumo ambao humfanya
kuwa na mali kama magari, nyumba na kadhalika. Mara nyingi mali hizo
huwa zinapatikana kwa mikopo na hutumia mshahara kulipia matumizi na
madeni, hasa kama madeni ni makubwa, mtu mwenye kipato cha kati anapaswa
kumuona mshauri wa maswala ya biashara. Hatua anazoweza kuchukua ili
kujikwamua na tatizo la madeni anaweza kulazimika kuuza baadhi ya mali
zake ambazo amezinunua kwa kutaka kuonyesha ufahari tu na ambazo hazina
umuhimu. Kwa mfano kama mtu ana magari matatu ya kutembelea, anaweza
kuuza magari mawili kubaki na gari limoja na fedha atakayoiokoa
kuiwekeza au kutumia kama mataji na kuanzisha biashara ili kujiongezea
kipato.
Mfumo wa mtu tajiri ni mfumo ambao unamwezesha kuwa na biashara yake,
kumiliki mali nyingi, kuwa na fedha nyingi katika akiba na awe
ameziwekeza kwenye vitega uchumi vinavyolipa faida kubwa zaidi ya
asiliamia kumi, kama vile nyumba za kupangisha na hisa. Mtu huyu hana
wasiwasi na maisha. Anaweza kusafiri au kuugua lakini vitegauchumi vyake
vinaendelea kumwingizia fedha. Siri kubwa ya matajiri ni uwezo wa
kutumia fedha na kuziwekeza kupata faida kubwa.
Hiki ni kitabu cha vitendo. Yote unayoyasoma humu inabidi uyafanyie kazi
ili yakusaidie. Tofauti kati ya maskini na tajiri iko katika kuchukua
hatua. Tajiri hujifunza mambo ya kumwendeleza na kuchukua hatua kwa
kutekeleza kwa vitendo yale anayojifunza na anayoyaona yanaweza kumuinua
kiuchumi. Maskini huwa anajifunza mambo na kuyaacha kichwani bila
kuchukua hatua au kuyafanyia kazi aliyojifunza na hivyo fursa ya kupata
utajiri inampita hivihivi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ReplyDeleteWELCOME TO THE GREAT BROTHERHOOD.
Do you want to be a member of Illuminati as a brotherhood
that will make you rich and famous in the world and have
power to control people in the high place in the worldwide
.Are you a business man or woman,artist, political,
musician, student, do you want to be rich, famous, powerful
in life, join the Illuminati brotherhood cult today and get
instant rich sum of. 2 million dollars in a week, and a free
home.any where you choose to live in this world
BENEFITS GIVEN TO NEW MEMBERS of ILLUMINATI.
1. A Cash Reward of USD $500,000 USD
2. A New Sleek Dream CAR valued at USD $300,000 USD
3.A Dream House bought in the country of your own choice
4. One Month holiday (fully paid) to your dream tourist
destination.
5.One year Golf Membership package
6.A V.I.P treatment in all Airports in the World 7.A total
Lifestyle change 8.Access to Bohemian Grove
account every month as a member
9.One Month booked Appointment with Top 5 world
Leaders and Top 5 Celebrities in the World.
If you are interested of joining us in the great brotherhood of illuminati CONTACT MR ROLAND or WhatsApp him +2348142587627
or email:illuminatipower666brotherhood@gmail.com