Tuesday, November 25, 2014
MBINU ZA MAFANIKIO KWA WAFANYABIASHARA
KATIKA haya mabadiliko ya milenia mpya, wajasiriamali wameweza
kujitofautisha na wafanyabiashara wakubwa ili kuwaridhisha wateja wao.
Kuwa na ujuzi, ustadi na uwezo wa kupigania kupata bidhaa bora ni njia
mahususi ya kufanikisha biashara.
Hivyo basi, mjasiriamali au mfanyabiashara mkubwa anatakiwa kuwa na
mipango mizuri na ya kitafiti kufanikisha hili, kwani huo ni ufunguo wa
mafanikio.
Mara nyingi mfanyabiasgara lazima awe mbunifu. Hivyo unatakiwa kuwa
mfikiriaji mzuri wa kuuza bidhaa unazozivumbua. Ni muhimu kuongeza
thamani katika bidhaa ulizo nazo na huduma zako.
Unapokuwa mjasiriamali unatakiwa kuwa na uvumbuzi wa mawazo yanayofanana
na biashara yako kwa kuongeza thamani au huduma. Kwa matokeo hayo
wateja watagundua ubora wakati watakapoona uhalisia wa bidhaa ulizo
nazo.
Unapotaka kuwa mfanyabiashara wa kiwango cha kuthaminiwa inakubidi uwe
mtawala mzuri na meneja aliyebobea.
Uwe hodari katika kujifunza na kupata faida ya teknolojia mpya ili iweze
kukusaidia kukuza biashara yako katika uchumi mpya. Kukamilisha
teknolojia mpya katika biashara yako ni lazima, hivyo utaendelea kukuza
na kuifanya iende na wakati.
Uwe mwendelezaji anayelenga kuimarisha mtandao. Kujihusisha na
wafanyabiashara wengine ni muhimu sana kwa kuwa itakusaidia katika
ukuaji wa biashara yako.
Pia kuwa mwangalifu kuimarisha mawasiliano uliyo nayo kwa wateja wako na
kujenga mawasiliano mengine mapya ili uweze kuwa na mazingira ya
kiushindani.
Baadhi ya mbinu za kufanya mabadiliko mazuri katika biashara yako ni
pamoja na uwazi, mpango wa kibiashara ulio wazi au unaoeleweka na
utaalamu. Uwazi unahitajika katika biashara yako, hivyo ni muhimu
kutozuia habari zozote muhimu na kuwa mkweli kwa wateja wako.
Kuwa na mpango wa biashara inayoeleweka kunakufanya uweze kuimarisha
ubora wa bidhaa na huduma, ili kufikia mahitaji ya wateja wako na
kuwaridhisha. Mpango wako wa biashara mara zote uwe unauangalia na
kuuimarisha uweze kuelewa mabadiliko na mahitaji ya wateja wako.
Unatakiwa kuimarisha na kutathmini utaalamu ulio nao ili kuweza kufanya
kilicho bora zaidi. Usisahau kwamba unahitaji kutoa muda ili kuzingatia
eneo lako la utaalamu ulionao.
Kumbuka matangazo na masoko kwa biashara ndogo yanaongeza bidii na
mipango ya kukuwezesha kufanikiwa zaidi. Wamiliki wengi wa biashara
ndogo ndogo wanavunjwa moyo kwa haraka kwa sababu hawaelewi upepo wa
biashara kwa wateja wao wanaowategemea baada ya kufanya kampeni ya
matangazo yao ya awali.
Matangazo ni sanaa inayokuwezesha kutazama na kutengeneza mpango wa muda
mrefu utakaokuongoza katika mafanikio.
Kuna mambo matatu wamiliki wa biashara ndogo ndogo wanayoweza kufanya
katika kuongeza nafasi ya mafanikio katika kampeni ya kutangaza.
Kwanza, unatakiwa kujiaminisha katika mpango wako wa muda mrefu. Kama
hukufanya hivyo bilashaka unahitaji mpango mwingine.
Jambo jingine ni kuwa unapokuwa na mipango ya kufungua biashara ni
matangazo. Kujitangaza ni njia moja nzuri sana, lakini nayo inahitaji
kuwe na hiyo mipango ya kujitangaza. Angalau unatakiwa kuwa na mpango wa
kutangaza biashara zako kwa miezi sita, lakini ukweli ni kwamba
inatakiwa ujitangaze kwa mwaka mzima. Hii itakusaidia kuimarisha mkataba
wa muda mrefu na watangazaji, kwani kwa kufanya hivyo utakuwa
unapunguza gharama za uangazaji.
Hii inakusaidia kufikia ukomo uliojiwekea wa uchapaji na kutoa ujumbe
mbalimbali unaotaka uwafikie wateja wako katika vipindi mbalimbali vya
mwaka.
Na jambo la tatu ni ongezeko la thamani - kama biashara ndogo
unashindana na ushirika wa wateja wako. Unatakiwa kuwa tofauti. Zungumza
kutokana na kile wateja wako wanachokihitaji na jinsi ya kuwapatia,
lakini pia unaweza kuwa sehemu ya wateja.
Inaweza kukuvunja moyo wakati unashindana na biashara ndogo na kubwa
endapo hutapata matokeo mazuri ya biashara kutokana na ulivyojitangaza.
Ili kuleta utofauti unayo nafasi kubwa ya kupata wateja wote ambao
hawakufanyi ukatulia.
Pata faida kwa kutoa huduma za bure – huduma za kawaida ambazo
wafanyabiashara wadogo wanashindwa kufaidika nazo ni kutoa taarifa kwa
vyombo vya habari. Kama una bidhaa mpya au huduma au kitu chochote kipya
katika kiwanda chako ambacho unafikiri kuwa wateja wako wanatakiwa
kujua, andika taarifa kwa vyombo vya habari. Pia unaweza kutoa taarifa
hiyo kwenye magazeti binafsi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment